COVID 19 - Our shipping update Read more *Important.

Natural Hair – Melanin fro Extensions

extensions za natural hair,

Natural Hair – Melanin fro Extensions

Kati ya styles zote duniani, si ajabu nikisema nywele nzuri kuliko zote ni za kwangu.. Glad I can say that to the world. Ninapenda sana hiki hiki kipilipili changu..hizi hizi nywele zinazofanana kama brush la bui bui (kama mama yangu anavyosemaga) –is my hair… and I love it. Nina furaha kwamba I have arrived kwenye hii state of mind na kama bado hujaanza kukikubali kipilipili chako I hope kuna siku utajiangalia na kusema nimeumbwa na nywele zangu hizi hizi nzuri na nitazipenda na kuzi thamini siku zote za maisha yangu. Sina haja ya kuzi suka kila siku, kuzi bana kila siku, kuna siku inabidi tu niziachie muone jinsi mungu ameniumba. Since huu mwaka uanze, I am in that state of mind! —– Au Naturale!!!! si mnakumbuka ule mtindo nilifanya miezi michache iliopita? ngoja niweke video hapa chini kuwakumbusha kidogo.

[ultimate_video u_video_url=”https://www.youtube.com/watch?v=KvoMVNd1tPU” yt_start_time=”525″ yt_stop_time=”576″ aspect_ratio=”4_3″ yt_autoplay=”on” yt_sugg_video=”” yt_mute_control=”” yt_modest_branding=”” yt_privacy_mode=”” play_size=”75″ enable_sub_bar=””]

Well! Sasa nimerudi na mtindo mtamu Zaidi!  Natural Hair- Melanin fro extensions! YESSS!!! Short story time maybe? Tulivyoanza kutengeneza nywele za Melanin Fro, tulikua tunatafuta match as close as possible to nywele ya Kitanzania. Yaani iwe natural hair haswa! Juhudi hulipa manake we have the best extensions in the market zinazoendana na nywele natural na zaidi pia hu- behave kama nywele natural meaning kuzisukia ni kujiongezea  a boost of length and volume!

Mtindo wenyewe sasa…

Mahitaji:

 1. Nywele : hutumia extensions zetu za melanin fro– inch 12 -Bunda mbili.
 2. Usukaji :  Tied Knots!!!
 3. Nywele zako ziwe safi, na uwe umezinyoosha kwa kuzifunga uzi, mabutu au twist siku kabla ya kusuka au uzi blow dry kabla. Na ziwe zina mafuta ya kutosha kwa sababu sio rahisi kukumbuka kuweka mafuta baada ya hapo.

The number of times nimeulizwa kama natural hair zinaweza kusukwa tied knots lol.  Mara nyingi mno! Na sikutaka kujibu kwa sababu moja tu—Inabidi nijaribu, nikae nazo kwanzaaa, kabla ya kutoa review yoyote au kuanza kuwasukia wateja wetu Kimz. This is how tumeanza, na ndivyo tunavyopendelea, we are our own guinea pigs and we love it!

Nilvyosukwa:

 1. Nilitaka kuachia nywele zangu pembeni kote (perimeter) kichwa kizima na upande wa mbele nimeacha mstari mwembamba Zaidi au kidogo sana. Hii ni kwasababu ukiacha nywele nyingi sana, tofauti zozote zilizopo zingeweza kuonekana kwa sababu nina nywele nyingi kwenye mizizi na binafsi kufanya hivi kumesaidia saana mtindo kuonekana natural zaidi.
 2. Niliomba kusukwa ndogo ndogo ili zijae. Kinky hair ndefu- zikiwa chache zinaweza kuonesha mapengo. Sikutaka ukiwa mbele uone through my hair (does it make sense?) na kwasababu nywele zangu sio ndefu mno nilijua zikishrink, huko mwishoni kwenye extensions mapengo yange onekana. But zikijaa sana, ninaweza tu kuzitrim au kuzi kata nikiona zimezidia! I was right!
 3. Nilichukua siku mbili, kila siku moja lisaa moja na nusu kwasababu wateja ni wafalme na wakifika saluni inabidi niwapishe wahudumiwe. So kwa size niliosuka pengine masaa 3 tuna estimate yanatosha.

Experience? -I love it! Love it, love it!-

Ninazipendea nini?

 1. Ninapenda ninavyoonekana nina nywele ndefu ya ki-Africa,
 2. Ninapenda zilivyojaa.
 3. Ninapenda zilivyo blend na my own natural hair.

Changamoto:

 1. Mtindo wa tied knots huchukua muda kwa ngozi kuachia baada ya kusukwa. Wakati wa kusuka maumivu hamna..msusi akivuta si unamwambia tu punguza..Ila ukisha suka kwa vile concentration iko pale kwenye root ya ngozi tu.. ngozi inakua rigid kidogo siku za mwanzo na depending na utafanya nini kuzi cool au ngozi yako au pain threshold yako, zinaweza kuachia haraka au zikachelewa. Personally nilikua napulizia maji ya baridi na kupaka mafuta ya mnyonyo (Black castor oil) mara kwa mara kutumia applicator bottle ili ngozi isikauke. (ngozi yangu huwasha ikiwa kavu). Siku 2 baadae nilijisikia vizuri afadhali na baada ya hapo siku zinavyoenda better and better! Day 4 I was GOOD!
 2. Daily fluff and Trim—sija mind hii sana kwasabu msema kweli mpenzi wa mungu, hata nywele zetu natural ukilala nazo bila ya kufunga mabutu n.k mziki wake tunaujua. Same goes for melanin extensions. Hizi extensions, zimetengenezwa kuungana kwa chini forming clusters zifanane na nywele asilia ya kiafrica zinavyoungana kwenye ends. So inabidi nizi fluff na kuzi trim kila siku to look neat. Ni kitu cha dk 5, no big deal.

Book hapa.

Matunzo:

 1. Zitie nywele zako binafsi unyevu pamoja na extensions. Nywele zako kwa vile ziko nje, usizisahau kamwe. Zi fluff pia kwa ndani la sivyo ukija kufumua unaweza kuta zimejifunga mno. Zipe unyevu kutumia mchanganyiko wa maji na leave in conditioner/ moisturizer yako yoyote uipendayo. Pia inasaidia extensions kushrink kwenda size ya kuaminika. Tumia trick hii kama haupendi muonekano wa big hair ukitoka kusuka tu, zi drench kabisa yaani zilowanishe kabisa na maji zitapungua volume kwa asilimia kubwa.
 2. Paka mafuta ngozi- Ngozi yako iko wazi ingawa imefunikwa na nywele, pakaa mafuta ili isikauke manake ngozi kavu huwasha, pia kuilisha ngozi vizuri ni moja ya chanzo cha afya ya nywele zako.
 3. Tifua na kata ncha kila siku- yess… fluff and trim daily! Kwanza hizi nywele ni kinky, ukilala na kuamka lowanisha na maji/ spray ya maji na uzitifue haswa mwishoni… punguza ncha kidogo na unaweza ku trim zile nywele zote ambazo hazikufurahishi.
 4. Usichane nywele.Yaani ninasisitiza, hakuna haja ya kuchana nywele isipokua tu kuzitifua. Kama unaona haja ya kuchana basi inaelekea  kwamba aina hii ya mtindo sio kwa ajili yako. The style ni Kinky, sio straight so iache iwe kinky, ukichana zitanyooka na hutaweza kuzirudisha hali ya viwimbi vya mbali kirahisi. So kuwa makini.
 5. Sio muhimu kudetangle nywele hizi kwa style hii. I know umeshtuka! Its contrary na ninavyosemaga kuhusu kudetangle your crochet braids. Hizi nywele originally zinakuja zimewekwa kimakundi, wakati wa kusuka, msusi atatenganisha anavyo chambua. Baada ya hapo atakapo zisuka zita form makundi zenyewe with time..unless unaweza kuzitenganisha kwenye hizo clusters zilizosukiwa, ukitenganisha sana zinaweza kutofautiana na nywele zako natural so kuwa makini sana, kuzi tifua au ku fluff kuna fanya kazi vuzuri tu. Zi detangle labda mara 1 kwa wiki au kwa siku 10.
 6. Unaweza kuosha. Swali lingine kubwa ni hili, “kama nina weza kuosha”. NDIO, unaweza kuosha mtindo huu, taratibu vizuri kutumia shampoo na conditioner… pakaa leave in conditioner kama kawaida na unaweza ku kausha nywele kutumia blow dry setting ya upepo. Setting ya moto itapunguza ujazo wa nywele maanake nywele zina asilimia kuwa ya kunyooka.
 7. Tumia satin bonnet, pillowcase au scarf wakati wa kulala, nywele zikisuguana na material nyingine zinazo nyonya unyevu huwa ni changamoto kidogo hivo jitahidi kuhakikisha kwamba unalilia au kuzifunika nywele kwa material hii.
 8. Utanogewa kukaa na nywele muda mrefu- tafadhali usifate huu ushauri wa kukaa na knots miezi 3 au sita. Kumbuka nywele yako ina pata uchafu, uchafu huu utajikusanya pale kwenye uzi wa knots kwasababu ndio hapo hamna movement yoyote…uchafu ukijikusanya kwa kiingereza tunasema it “mattes” yaani inajikusanya kama gundi…wengi hupoteza nywele hapo..kufumua hio gundi ya uchafu! kukaa nazo sawa utadumu muda lakini “is it worth it?” kama mwisho wa siku utapoteza mkono umejaa nywele? Kwangu hapana. Tujifunze kukaa na nywele muda ulio reasonable.. hata kama extensions zinafika huo muda…epuka kukaa na nywele yoyote muda mrefu kiasi hicho kama unapenda afya ya nywele zako. For me mwezi na nusu ni reasonable time nikikaa nazo sana. Miezi miwili tayari naanza kua na wasiwasi. Fanya hii test kuangalia ni kipindi gani nywele yako ilikatika sana… ulipokaa nayo wiki 2 au miezi 3? Then niambie kwenye comments..

Suggestions:

Kama uko concerned na nywele yako kubaki wazi kipindi chote una uwezo wa kuzifunga twists nywele zilizobaki nje haswa kama haubani. Hizi twists unaweza kuzifunga baada ya kusuka knots. Hii njia haitafaa watu wote. Kwasababu extensions ni voluminous twists hazionekani but sio kwa kila mtu kwa maana tuna nywele tofauti. Cha msingi ni do not deal na nywele zako zikiwa kavu yani step 1 ni kuzipulizia maji au mchanganyiko wetu kisha ndo uzi fluff n.k.

Gharama za Kusuka knots Kimz- Salon

 1. Nywele – Wastani 2 pcs @14,000/=: 28,000
 2. Ususi knots – 80,000/=

Wastani jumla = 108,000/=

Book hapa.

mara baada ya kumaliza kusuka.

well that’s all ndugu zangu. Asanteni kwa kutembelea blog yetu, tukutane kwenye post nyingine.

Mapendo Tele

-Nice-

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *